SMS: Jinsi ya Kumvutia Mwanamke Kupitia Simu Yako!


Unataka kumvutia mwanamke unayemzimia kupitia SMS? Sio lazima uwe mshairi au mchekeshaji mkuu! SMS tulizoziorodhesha hapa sio za kutongoza moja kwa moja, bali zinakusaidia kuanzisha mazungumzo yenye maana na ya kuvutia.

Siri ya Mafanikio: Hakikisha unatumia SMS hizi kama kichocheo cha mazungumzo, sio kama script ya kufuata. Kuwa mkweli, msikilize, na uonyeshe kuwa unamjali.

Maswali 20 ya Kukufanya Muongee kwa Masaa:

  1. Ni kitu gani ushawahi kufanya, lakini hautafanya tena? Swali hili linamfanya afikirie kwa kina na unaweza kugundua mambo mnayoshirikiana.
  2. Tabia gani ya ufidhuli ambayo uko nayo? Kila mtu ana tabia yake ya kipekee. Kumruhusu aeleze yake kunamfanya ajisikie huru zaidi kuongea na wewe.
  3. Rafiki yako wa dhati ni nani? Rafiki zake ni muhimu. Jihusishe na rafiki yake ili kuimarisha uhusiano wenu. Uliza walikutana lini na jinsi gani.
  4. Ni jambo/kitu gani ulichofanya kitambo ambacho ungetamani usingekifanya? Kufanya makosa ni sehemu ya maisha. Akiweza kulijibu swali hili, inamaanisha anakutrust.
  5. Kitu gani unachoogopa zaidi? Ukijua uoga wake, unaweza kuwa mwangalifu na kumkinga. Anakupa ruhusa ya kumtunza.
  6. Sehemu gani hapa ulimwenguni ungetamani kuishi? Swali hili linamruhusu awe mbunifu na kueleza hisia zake. Pia, unapata kujua matamanio yake na unaweza kupanga date sehemu anayoipenda.
  7. Ungependa kuchagua pesa au mapenzi? Jibu lake litakuambia mengi kuhusu vipaumbele vyake.
  8. Kumbukumbu ipi ya utotoni mwako unaipenda? Kumbukumbu za utotoni huleta furaha. Tafuta kujua mambo yaliyomfurahisha zamani.
  9. Ni jambo gani la aibu zaidi ushawahi kufanya? Mambo ya aibu huchekesha. Tumia fursa hii kumfanya acheke.
  10. Deti ya ndotoni mwako unapenda ingekuwa vipi? Swali hili ni zawadi! Tumia jibu lake kupanga date ya kusisimua.
  11. Kitu gani ungependa kubadilisha maishani mwako? Kujua udhaifu wake kutawafanya muungane.
  12. Nani amekuwa mshawishi mkuu katika maisha yako? Jibu lake litakufahamisha kuhusu maadili yake. Mama yake? Yeye ni wa kuoa!
  13. Ni vitu gani ulikuwa ukipenda kufanya ukiwa utotoni na ungependa kufanya sahizi? Swali hili linafungua moyo wake. Tumia fursa hii kumfurahisha.
  14. Kitu gani unachukia katika deti? Epuka makosa madogo madogo kwa kuuliza swali hili.
  15. Maisha yako ya mbeleni unataka yaweje? Jua mipango yake ya baadaye. Je, mnaendana?
  16. Je uko karibu na familia yako? Uhusiano wake na familia yake unaweza kuonyesha tabia yake.
  17. Filamu gani imekushawishi zaidi? Filamu anazozipenda zinaweza kuonyesha tabia zake.
  18. Sehemu ambayo unaiona salama zaidi maishani mwako ni wapi? Kujua mahali anapojisikia salama ni muhimu.
  19. Ni kitu ama jambo gani ambalo ungependa kufanya kabla hujafa? Swali hili litamfungua zaidi na unaweza kumsaidia kutimiza ndoto zake.

Muhimu: Usisahau kuwa wewe mwenyewe! Kuwa mkweli na ufurahie mazungumzo. Bahati njema!

Comments

Popular posts from this blog

mbinu za ngono na mwanamke

Mwanaume mzee zaidi: Ishara 7 kwamba anataka uhusiano wa kudumu

Maneno 50 Ya Kumwambia Mwanamke Ili Moyo Wake Usisimke